picha

MALAS ADVENTURES COMMUNITY

We

Huduma zetu
logo

Karibu MALAS ADVENTURES COMMUNITY

Hello! Karibu katika familia ya MALAS ADVENTURES. Mahali ambapo tunaangazia vivutio vya utalii, maeneo ya kuhistoria na utamaduni. Tunajihusisha na uandishi wa makala za utalii, kuandaa picha na video za vivutio mbalimbali katika kila kona ya dunia.

Kwetu kujifunza na kuangazia maeneo mengi ya dunia ni jukumu letu. Napenda kukukaribisha katika jumuiya ya waandishi, watafiti, na wafuatiliaji wa makala za utalii, utamaduni, wanyamapori, mazingira, na tabia-nchi.

Kwenye tovuti yetu utajifunza mambo mengi sana na mazuri kuhusiana na utalii, wanyamapori, viumbe bahari, na ndege wa angani. Pamoja na hayo yote, utaweza kujifunza namna gani ya kukabiliana na viumbe hatarishi pale unapokuwa kwenye hatari kama vile nyoka, simba, kiboko, na wengineo wengi ambao kwa muda mrefu historia ya mwanadamu imekuwa na hofu pale kunapokuwa na muingiliano wa kimazingira na hawa wanyama.

Hivyo usiwe na shaka tena kwa kuwa vijana wazalendo wapo mstari wa mbele kukuletea njia zenye usalama pindi uwapo kwenye hatari. Kubwa zaidi ni tunaangazia maeneo mengi sana duniani na yenye mvuto kama milima, maporoko ya maji, bahari, na mbuga.

Usikae mbali nasi. Karibu tujifunze na kufurahia uzuri wa Dunia yetu kwa pamoja.

soma zaidi

Kazi za MALAS ADVENTURES COMMUNITY

Malengo yetu makubwa ni kuwa kiunganishi kwenye utalii na utamaduni. Katika kutimiza hilo MALAS tunatekeleza majukumu yafuatayo;

Kutangaza vivutio vya utalii Tanzania

Hifadhi za wanyamapori, maeneo ya kale, utalii bahari, na utalii wa anga.

Kuandaa na kuandika machapisho mbalimbali

Kuandika vipeperushi, vitabu, makala, zinazogusia utalii na utamaduni.

Kuwa kiunganishi kwa watalii.

Tunafanya huduma za ushauri wa sehemu bora za kutembelea kwa majira husika.

Kuratibu safari za kitalii kwa shule na makundi mbalimbali ya kijamii

Tunaandaa safari za kutembelea ofisi, taasisi, na mashirika ndani ya Tanzania.

Tunayo angazia

Utalii Tanzania

Tanzania imesheheni vivutio vingi vya utalii, maeneo ya kupumzika na kumbi za mikutano. Yote hayo utayapata hapa kwa undani.

Wanyamapori

Twiga ana madaha ya aina yake, simba na ufalme wake, tai na anga lake, duma na mwendokasi, na wanyama wengineo wote utawafahamu mahali hapa. Kaa mkao wa kula maarifa bora.

Watu na Tamaduni

Tunaishi kwenye dunia yenye watu wa namna mbalimbali, tamaduni mbalimbali na zenye kuvutia pia. Tujifunze tamaduni za jamii mbalimbali karibu kila bara.

Mazingira

Tunaangazia namna bora ya kutunza mazingira yetu. hatujaacha nyuma tabia-nchi na hali ya hewa. Dunia yetu, mazingira yetu, Uhai wetu.

Viumbe bahari

Bahari ni zaidi ya maji, samaki, nyangumi. Hayo ni machache tu, kuna uzuri wa kipekee katika utalii wa bahari ambao unajumuisha uzuri usio kifani.

World Heritage Sites

Maeneo ya Urithi wa dunia yana historia muhimu inayogusa dunia na maisha ya mwanadamu. Karibu tujifunze zaidi.

Historia ya MALAS ADVENTURES COMMUNITY

MALAS Adventures Community (MAC) ilianzishwa mwaka 2021, lakini wazo lilianza mwaka 2018 ambapo ilikuwa ni ukurasa mtandao wa Facebook uliozungumzia athari za ujangili pekee. Mwaka 2021 ndipo ilianzishwa rasmi na kuanza kupata wanachama, wakati huo inaitwa WILDLIFE AMBASSADOR. Mwaka 2024 jina lilisajiliwa BRELA na baadae jina liliboreshwa na kuitwa MALAS ADVENTURES COMMUNITY

Picha

picha
picha

Vijana katika banda la utalii, Chinangali.

picha

Wanachama walipotembelea ofisi za TTB Dodoma

picha

Wanafunzi katika ofisi za TTB Dodoma

picha

Wanafunzi katika ofisi za TTB Dodoma

picha

Wanafunzi katika ofisi za TTB Dodoma

picha
picha

kampeni ya VOTE NOW

picha
picha
picha

MALAS timu katika picha

picha

MALAS timu ofisi za TTB

picha

Banda la Ngorongoro, Chinangali

picha

kampeni ya VOTE NOW

picha

Mawasiliano

Anuani

Dodoma, Tanzania

WhatsApp

+255 741131114

Email

malascommunity7@gmail.com

office@malas.co.tz